SHURBA YA NYAMA YA MBUZI
Vipimo
Nyama ya mbuzi 2LB
Nyanya 1
Kitunguu maji 1
Kidonge supu 1
Maji 4 mugs
Kitunguu thomu kijiko supu 1
Bizari pilau kijiko chai 1
Bizari manjano nusu kijiko chai
Mdalasini kijiti 1
Shairi ( oats) vijiko supu 5
Pilipili mbichi 2
Ndimu/siki ya zabibu vijiko supu 2
Chumvi kiasi
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA
OSHA nyama vizuri tia kwenye sufuria
Katakata kitunguu maji na nyanya
Tia kidonge supu,mdalasini,chumvi na maji,funika chemsha nyama hadi iwive.
Tia oats kwenye bakuli na maji iache nusu saa kisha isage kidogo tu na mimina kwenye supu ya nyama
Tia pilipili mbichi mzima,thomu bizari zote na siki.
Weka moto mdogomdogo huku unakoroga kila baada ya muda
Tazama uzito na ongeza maji kidogo ukihisi ni nzito.
Hapo tegua tayari kwa mlo wako
Hakuna maoni