Welcome.

Karibu Katika Blog Ya Appo Power. Pia karibu katika group letu la WhatsApp APPO POWER GROUP. Daily Walk

SUPU YA KUKU NA VIAZI MBATATA

Vipimo

Kuku 4LB
Viazi mbatata 3
Kitunguu maji 1
Kitunguu thomu chembe 5
Pilipili mbichi 2
Nyanya ya kusaga kijiko chai 1
Pilipili manga kiasi
Holdi/Tumeric/bizari manjano kiasi
Mafauta ya zaituni vijiko vya supu 2
Kotmiri msongo 1
Ndimu/Siki vijiko supu 2
Chumvi kiasi

NAMNA YA KUANDAA NA KUPIKA
Osha kuku mkate vipande kiasi unachohitaji
Menya viazi mabatata katakata vipande unavyohitaji
Menyw kitunguu maji vipande vidogo vidogo ukate
Weka mafuta katika sufiria lililokwenye jiko lililowashwa moto kisha tia kitunguu maji na vikaange kiasi hadi vilainike kisha tia vipande vya kuku,chumvi,pilipili manga ,thomu.

Tia nyanya Holdi na maji kiasi

Tia viazi mbatata na uwache vichemke na kuku hadi viwive kwa pamoja

Katakata kotmiri na pilipili mbichi utie mwishoni

Tia ndimu kisha tegua hapo ipo tayari kuliwa.

Unaweza kutumia kwa chakula upendavyo

Mchana mwema na mlo mwema na supu yako.

Hakuna maoni