UJANA NA MATENDO
Muhali gani wapendwa wa Appo Power nitumaini letu muwazima wa afya.
Lengo nikuzungumzia kuhusiana na ujana na matendo yanayotendeka kupitia wakati wa ujana hadi kuzeeka ima kufa.
Ujana ni mapito ya kila mwanadamu anaeanzia utoto akiwa na siku moja hadi kufikia kubalehe kua na matamanio ya kufanya maamuzi anayojisikia mwenyewe bila kuangalia athari na faida yake.
Hapa ndio tunaposema unaanzia ujana kwani tayaari unaanza kubadilika kimwili na kukabiliana kwa kila hali ya kimwili na kimazingira.
Waswahili husema ujana maji ya moto hii hudhihirika pale vinapoanza vitendo visivyostahili kutendeka kwa vijana mfano kujiingiza kwenye vigenge viovu kama kuvuta bangi,kujiingiza kwenye anasa na mengineyo mengi
Ujana humfanya kijana ajione anafanya sawa kila analolitenda na kutokusikiliza wakubwa zake wanachomshauri.mwisho wa siku akifikia karibia uzee wake
ndipo anapojua ameutumia vibaya ujana wake.
Ukumbusho kwa vijana: Utumie vizuri ujana wako ili upate faida na ustarehe uzeeni kwako.
Hakuna maoni