FAIDA ZA ZABIBU KIAFYA
Zabibu ni matunda matamu yanayopendwa yakiwa na faida nyingi kiafya katika mwili wa mwanadamu.
Kuna zabibu ranging nyekundu,nyeusi, na rangi ya kijani.
Unaweza kula zabibu kama matunda zabibu zilizokaushwa(raisin) au kama juisi pia.
Zabibu hutumika sana kutengeneza mvinyo ( wine), sehemu mbali mbali duniani.
FAIDA ZA ZABIBU KIAFYA
Kusaidia kuondoa kukosa choo,mmengenyenyo wa chakula kwenda vizuri kupunguza uchovu na kuzuia mtoto wa jicho pia.
VIRUTUBISHO VILIVYOPO NDANI YA ZABIBU
Kilogramu 100 za zabibu zina wastani ya virutubisho vifuatavyo
1.Nishati kilokaro 69.
2.Wanga gramu 18.1.
3.Sukari gramu 18.1.
4.Kamba lishe gramu 0.9.
5.Mafuta gramu 0.16.
6.Protini gramu 0.72.
ZABIBU PIA ZINA VITAMIN ZIFUATAZO
Vitamin B1,B2,B3,B5,B6,B9
Vitamin C
Vitamin E
Vitamin K
Pia zabibu zina maadini
Kalsiam mg 10
Chuma mg 0.3
Magneziam mg 0.71
Sodium mg 2
Potassium mg 191
Fosfaras mg 20
FAIDA ZA KIAFYA
Ulaji wa zabibu katika mlo wako,una faida nyingi kiafya, zikiwemo.
KUTIBU PUMU
Zabibu zinasaidia kuongeza unyevunyevu katika njiwa ya hewa na hivyo zinapunguza utokeaji wa pumu.
HUIMARISHA MIFUPA
Madini ya shaba,chuma na manganese yanapatikana kwa wingi
Katika zabibu,ambapo madini haya
ni sehemu ya kujenga mifupa imara na yenye afya. Kula zabibu mara kwa mara kunasaidia kupunguza kutokea kwa mifupa kulainika kutokana na umri pamoja na kuimarisha mifupa,madini hayo pia,husaidia mwili kufanya kazi vizuri.
Zabibu hupambana na magonjwa ya moyo
Zabibu huongeza nitric oxide katika damu,ambayo huzuia damu kuganda,husaidia kuzuia mafuta kujirundika/kujikusanya katika mishipa ya damu, na ina kampaundi za flavonoids aina ya resveratrol na quercretin ambazo husaidia kutoa sumu mwilini.
Yote haya husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo,na shinikizo la damu.
Zabibu husafisha figo
Zabibu zina viondoa sumu ( antioxidant) ambazo husaidia kuondoa sumu (free radicals) kutoka kwenye figo,pia hupunguza tindikali ya wiki ( uric acid) kwakuongeza kiasi cha mkojo unaotengenezwa na figo
Kupunguza lehemu ( Cholesterol)
Zabibu zinaweza kupunguza lehemu kwenye damu.
Zina kampaundi kama pterostilbene,ambazo zinadhaniwa kupunguza mafuta ya lehemu kwenye damu.
Pia aina ya kampaundi iliyomo kwenye ngozi ya zabibu ziitwazo saponins, hizi hipinguza unyonyaji wa lehemu kutoka kwenye utumbo
Kupunguza hatari ya kupata saratani
Kampaundi zinazopatikana katika zabibu kama resveratrol,husaidia kuondoa sumu,zinazoweza kuleta saratani mwilini.Baadhi ya kampaundi nyongine huzuia seli za saratani kukua na kauzaliana
Zinaimarisha mfumo wa kinga ya mwili.
Zabibu zilizokaushwa zina faida nyingi kama kuzuia choo kigumu homa na kuongeza damu.
Unaweza kutengeneza juice ya zabibu na unachanganya na tunda gani ili iwe pouwa
JibuFutaHili ni swali zabibu kavu nisage na nini ili ninywe km juice?
JibuFuta