Welcome.

Karibu Katika Blog Ya Appo Power. Pia karibu katika group letu la WhatsApp APPO POWER GROUP. Daily Walk

Hatua za maisha

Muhali gani wapendwa wa Appo Power tunatumai muwazima wa Afya na furaha tele ikiambatana na amani miyooni mwenu.

Leo katika neno letu tutazungumzia kuhusiana na hali za maisha na jinsi tunavyoishi.

Maisha ni safari isiyokua na uhakiaka ikiwa na maana
ya  kwamba katika maisha kuna mabonde,milima,misitu,mito na misitu yenye wanayama wakali ikimaainisha kwamba kuna kupanda na kushuka,furaha na kilio.

Maumuvu nimiongoni mwa hatua za maisha hapa kinachotakiwa nikuishi kwakumtegemea Mungu na kuwa na subira ukiamini kila hatua unayopitia inamakusudio yake.
Hiii ndio inayoleta maana ya maisha kuwa ni safari ndefu.

Katika maisha kuna hali tofauti
-kuna wenye hali mbaya
-kuna wenye hali katinakati
-kuna wenye hali nzuri

Hivyo ikimaanisha kuna masikini wasiojua muelekeo,kuna wakawaida wanakua na wastani wa maisha na kuna matajiri wanaopata mahitajio yao kwa wakati.Aidha tunaona kuna wenye Afya njema na kuna wagonjwa.

Hapa kuna baadhi yetu tunajiona tumefika katika hali Fulani huku tukiwadharau wenzetu tukiamaini tulipo hatuwezi kushuka ikiwa ni Mali au kiafya huku tukisahau alietupa hiyo hali anaweza kutupokonya akampa mwenginewe
Kama alivyotuumba na anaweza kutushusha kwa kutupatia kifo au Maradhi au ufukara.

Tunachotakiwa kila mmoja wetu amathamini mwenzake huku akiamini ipo siku anaweza kushuka ama anaweza kupanda

Katika kila hali tunatakiwa kuheshimina,kuthaminiana na kupendana hali fulani isitufanye tukawekeana matabaka sote niwamoja.

Shukrani kwa kuwa nasi mwanzo hadi mwisho wa neno letu la leo

Hakuna maoni