MAKANDE
vin IMO
Nyama vipande vidogo vidogo nusu kilo
Mahindi vikombe 2
Maharage vikombe 3
Kitunguu maji 1
Nyanya 2
Kabichi lilokatwakatwa vikombe 2
Kitunguu thoumu kijiko cha chai 1
Vidonge cha supu 2
Chumvi kiasi
Mafuta ya kula kiasi
KUTAYARISHA
Chemsha mahindi yawive hadi yakauke maji kidogo
Chemsha maharage yawive hadi yakauke maji kiasi
Tia mafuta ndani ya sufuria kisha tia vitinguu maji na thomu pamoja na vidonge vya supu
Tia nyama iliyokatwa acha ikaangike kidogo na chumvi
Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo hadi nyama iwive
Mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa pamoja na maji yake koraga mchanganyiko kisha tia kabichi funika hadi kabichi iwive onja chumvi kama nikiasi
Kisha subiria ikauke kwa kukoroga mchanganyiko wako ikiwa tayari weka ndani ya sahani tayari kwa mlo wako.
Natumai unafurahia mapishi ruhusa kumeza mate mlo wetu tayari tunakula Appo Power.
Hakuna maoni