Welcome.

Karibu Katika Blog Ya Appo Power. Pia karibu katika group letu la WhatsApp APPO POWER GROUP. Daily Walk

CHOROKO ZA KUPAAZA ZA NAZI

Vipimo
Choroko za kupaaza kikombe kikubwa ( mug) 1
Kitunguu maji 1
Binzari ya manjano ya unga nusu kijiko cha chai
Kitunguu thomi 1
Nyanya 1
Pilipili nzima 1
Nazi 1-2
Chumvi kiasi

JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA
 
*Osha choroko kwa maji vizuri kisha zichemshe kwa kutia maji kiasi ili ziwive na zisivurugike
*katakata kitunguuaji vipande vidogovidogo
*Menya nyanya na uisage.
*Weka sufuria jikoni na moto kiasi,kisha weka mafuta ya kula au siagi au samli kiasi.
*kaanga vitunguu mpaka vibadilike rangi kidogo.
*Tia bizari ya manjano kaangia kidogo.
*Tia thomu kaangia kidogo.
*Tia nyanya ulioisaga na chumvi.
* koroga mchanganyiko  kama dakika 5-10.
*Mimina choroko zilizochemshwa changanya wacha maji yakauke kiasi.
*Mimina tui la nazi koroga onja chumvi na punguza moto wacha ichemke tui na kufanya rojo kidogo
Ili upate rojoro.
*Katia pilipili ziwive kiasi kisha tegua.
Hapo tayari weka kwa bakuli na unaweza kulilia wali,chapati,na mikate mbalimbali.

Hakuna maoni