Welcome.

Karibu Katika Blog Ya Appo Power. Pia karibu katika group letu la WhatsApp APPO POWER GROUP. Daily Walk

KUONDOA CHUNUSI KWA KUTUMIA MVUKE NA LIMAO/NDIMU

CHUNUSI
Ni jamii ya vipele vinavyokua sugu katika ngozi ya mtu hususan usoni,mgongoni na hata katika makalio.
Pia chunusi hutokea au huota.

SABABU ZA KUOTA CHUNISI

Mpendwa wa Appo Power kabla ya kuondoa chunusi lazima ujue sababu zinazopelekea kuota chunusi.

-Balehe: haya niabadiliko ya mwili kutoka hali ya utoto kwendea ujana,hapa ndio hutokea chunusi na mara nyingi chunusi zinazotokea hapa baada ya mda hupotea.

- Matumizi ya vipodozi/Mafuta yasioendana na ngozi yako.

- Vyakula vyenye mafuta/protini kwa wingi kama kutumia karanga, chunusi ni matokeo ya mafuta yaliyojikusanya na kuiva katika ngozi ambao vijitindu vilijiziba.

-Kutosafisha uso mara kwa mara
Unatakiwa kusafisha uso mara 2 au 3 kwa siku yaani akiamka na kabla ya kulala. Hii itasaidia ngozi kuacha vijitundu kupumua kwa urahisi na visizibe.

VIFAA
- Ndimu/Limao
- kitambaa safi na laini
- Maji moto
- Beseni dogo
-Taulo kubwa kiasi

HATUA
- Chemsha maji na uweke kwa beseni,hakikisha yanatoka mvuke ambao ndio unaohitajika.

- Jifukize mvuke sehemu zenye chunusi kama ni usoni fanya kuinamia beseni huku ukijifunike taulo ili mvuke usitoke nje ya uso.Inama ukiwa hivuti hewa kisha inuka kuvuta hewa.Zoezi hili litachukua dakika 5-10

- Jifute vizuri kwa taulo sababu kutakua na jasho hapo,kisha chukua limao kamua katika chombo safi na tumia kitambaa laini kupaka usiguse ila paka taratibu.Kisha kaa kwa dakika 10-15 tena osha uso kwa maji safi pakaa mafuta yanayoendana na ngoziyako.

SHERIA
Zoezi hili ni kwawale walio na ngozi ya mafuta ikiwa ngozi yako ni dry usitumie mvuke pakaa limao tu.

Hakuna maoni