Muhogo,Samaki wa kuchoma na Bamia
VIPIMO
Mihogo (fresh) 3-4
Tui la kopo (box) 1000ml
Chumvi 1 kijiko cha chai
Kitunguu maji kilokatwakatwa 1
Nyanya/tungule 3-4
Pilipili mbichi ndefu 2-3
Pilipili boga 2
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Menya Mihogo kisha ikate vipande inchi tatu hadi nne,kila kipande kigawe kitoke vipande vinne,kisha to a mizizi katikati.
Osha vipande vya Mihogo ipange ndani ya sufuria ya nafasi na yenye mfuniko,ili upate nafasi ya kutia viungo vyake ulivyoviandaa.Pia utoaji wa tui wahitaji nafasi.
Tandaza kitunguu maji,nyanya,pilipili boga na pilipili mbichi juu ya sufuria lenye vipande vya mihogo, tia chumvi na tui lote.
Funika sufuria kisha weka jikoni moto wa kiasi kuchemsha tui lipande juu.Hakikisha tui halifuriki na kumwagika kwa kuchungulia au kufunika nusu mfuniko kwa mda wa nusu saa,ukiona tui linatokota chinichini funika mfuniko na upunguze moto mdogo kabisa tui likauke kidogo liwe zito
BAMIA/MABENDA
VIPIMO
Bamia robo kilo
Nyanya 3
Kitunguu maji
Kitunguu saumu(thomi/galic) ya unga au ilosagwa 1kijiko cha chai
Mafuta150ml
Chumvi 1 kijiko cha chai
Pilipili boga
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Kata vichwa vya bamia kisha zikate kate mara mbili zikiwa kubwa,ikiwa ni ndogo osha tu uweke kando.
Katika sufuria katakata kitunguu maji,nyanya,pilipili boga tia ndani viungo hivi ongeza chumvi,mafuta,thomu na nyanya kopo.
Washa moto mdogo mdogo huku umefunika sufuria kwa muda wa dakika 20 kisha ukiona mboga zimeshika kutokota ongeza bamia
Koroga.
Tia maji 200ml wacha kwa muda wa dakika 15 kupika tena,ukionja utamu wa mboga na chumvi hakikisha bamia pia zimewiva tayari kuliwa.
SAMAKI WA KUCHOMA
VIPIMO
Samaki (Dorado) au mikizi au 2 wakubwa (fresh)
Chumvi 1kijiko cha chai
Kitunguu saumu( thomi/galic) ya unga au iliyosagwa 1 na nusu kijiko cha chai
Tangawizi mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supu.
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUCHOMA
Safisha samaki vizuri mchane chane kwa ajili ya kuweka masala.
Changanya viungo vyote na chumvi kisha paka katika samaki kote ndani ya sehemu ulizochanachana,mroweke kwa muda wa robo saa hivi.
Weka karatasi ya jalbos ( foil paper) katika treya ya Oven. Muweke samaki kisha mpike (grill)achomeke hadi samaki ageuke rangi na awive.
Kufikia hapo andaa mezani muhogo samaki wa kuchoma na bamia kwa ajili ya kula na familia.
Hakuna maoni