Welcome.

Karibu Katika Blog Ya Appo Power. Pia karibu katika group letu la WhatsApp APPO POWER GROUP. Daily Walk

TENDE YA KUSONGA YA LOZI NA CORNFLAKES

Vipimo

Tende zilizokatwa katwa kwa kutolewa kokwa 1 kilo
Cornflakes 1na nusu kikombe
Lozi zilizokatwa katwa 1 kikombe
Siagi robo kilo

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  Mimina tende na siagi ndani ya sufuria bandika motoni,moto mdogo mdogo hadi zilainike kwa muda wa dakika kumi.

  Isonge kidogo kwa mwiko ili kuchanganyika vizuri.

Changanya cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyike vizuri.

Paka mafuta au siagi ndani ya treya au sinia.

Mimina mchanganyiko wako ndani ya sahani au treya,kisha zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda.

  Hapo tayari tende ya kusonga ya lozi na cornflakes zinaweza kuliwa kwa kahawa.

Maoni 1 :