Welcome.

Karibu Katika Blog Ya Appo Power. Pia karibu katika group letu la WhatsApp APPO POWER GROUP. Daily Walk

SUPU YA MAHINDI,KAROT NA VIAZI

Vipimo
  Karoti( katakata ndogondogo)3.
  Viazi  ( katakata vidogo vidogo- cubes) 3.
   Mahindi ( chembe ) 2 vikombe.
    Supu ya vidonge ( stock - maggi cubes) 1kidonge.
    Pilipili manga kijiko cha chai 1.
    Chumvi kiasi.
    Ndimu kijiko cha chai 1.
    Siagi au mafuta vijiko vya supu 2.

Jinsi ya kutayarisha na kupika
     - Tia siagi au mafuta katika sufuria,kaanga viazi vikiwa tayari kiwiva tia karoti,endelea kukaanga kwa dakika tatu.
     -Tia mahindi changanya katika moto mdogo.
    -Tia maji kiasi,tia kidonge cha supu ( stock),tia pilipili manga,chumvi na ndimu.
   -Acha ichemke hadi viazi viwive vizuri.
  -Saga nusu yake ndani ya blender kisha rudisha kwa sufuria kisha changanya pamoja.
  -Mimina katika bakuli ikiwa tayari kuliwa.

Hakuna maoni